Mufti:''Twitter ni chanzo cha maovu''

Image caption Mufti Sheikh Abdul Aziz al-Sheikh anasema Twitter imejaa taarifa za uongo na zisizo na msingi

Mtandao wa kijamii wa Twitter unaosifika sana miongoni mwa wanawake na wanaume nchini Saui Arabia, umesemekana kuwa chanzo cha maasi na uovu.

Hii ni kauli ya mufti mkuu wa Sadi Arabia katika taarifa kwenye mtandao wa 'Al Arabiya news'.

''Ikiwa mtandao huo ungetumiwa kwa njia inayostahili , ungekuwa na manufaa makubwa kwa jamii, lakini badala yake mtandao huo unatumika kwa mambo ya kipuuzi.''

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Twitter hutumiwa na watu wengi kupashana habari kote duniani

Alisema sheikh Abdul Aziz al-Sheikh katika kipidni chake cha televisheni kiitwacho Fatwa siku ya Jumatatu.

''Twitter ni chanzo cha maovu na uharibifu,'' alisema Mufti huyo.

''Watu wanakimbilia mtandao huo wakidhani ni sehemu ya kupata taarifa za uhakika wakati mtandao huo umejaa uongo na porojo tupu,'' aliongeza kusema Mufti huyo.

Saudi Arabia hutumia sheria za kiisilamu ikiwemo kuwatenga wanaume na wanawake , hali ambayo ndio msingi wa mfumo wa maisha katika ufalme huo.