Apigwa mawe kwa ubakaji Somalia

Image caption Al-shabaab wanafuata sheria kali ya kiisilamu

Kundi la Al Shabaab limempiga mawe hadi kufa mwanamume mmoja nchini Somalia.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 alipigwa mawe Jumanne eneo la Lower Shabelle Kusini mwa Somalia.

Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi ya ubakaji iliyomhusisha mwanamume huyo alisema alipatikana na hatia ya kumbaka mwanamke akiwa amejihami kwa bunduki.

Al-Shabaab hutumia sheria kali ya kiisilamu au Sharia kutekeleza sheria na mwezi jana mwanamke mmoja pia alipigwa mawe hadi akafariki kwa kufanya zinaa mjini Barawe.