Ebola kukwamisha AFCON?

Haki miliki ya picha CAF
Image caption Moroko

Ugonjwa wa Ebola umesababisha kutokuelewana kati ya Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika CAF na mwenzake wa UEFA.

Msuguano huo unakuja baada ya Rais wa UEFA Michel Platini kutoa maoni ambayo yalishauri Shirikisho la Soka la Afrika kuwasiliana na Shirika la Afya Duniani kuhusiana na michezo AFCON nchini Moroko.

Hata hivyo malengo ya mawasiliano hayo ili kuona hatari ya Ugonjwa wa Ebola iko kwa kiasi gani na ikiwezekana mashindano ya AFCON ya mwaka ujao yaahirishwe.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Serena Williams

Nae Serena Williams mwenye miaka 33 amepata kipigo ambacho kwa mara ya mwisho alikuwa na umri miaka 16.

Kipigo hiki kipya cha seti 6 - 0, 6 - 2 amekipokea kutoka kwa mwanadada wa kiromania Simona Halep mwenye miaka 23.