Simona Halep aendeleza vipigo

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Serena Williams

Baada ya Simona Halep kumshushia kichapo cha seti 6-0 6-2 Serena Williams amezinduka na kumbamiza mcanada Eugenie Bouchard kwa Seti 6-1 6-1.

Ushindi huo unampa matuamaini Serena angalau kuifikia nusu fainali na unayafuta matumaini ya Euginie katika michuano hiyo inayofanyika Singapore. Lakini huenda Serena Williams asiende mbali iwapo Ana Ivanovic atampiga Simona Halep katika mchezo wa leo hii.