Gesi chafu kupunguzwa hadi ifikapo 2030

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mabadiliko ya hali ya hewa

Viongozi wa Muungano wa Ulaya wanaokutana mjini Brassels wamefikia mkataba muhimu kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ambapo wameazimia kupunguza kiwango cha asilimia arobaini ya gesi chafu kufikia mwaka 2030 ikilinganishwa na viwango vya mwaka 1990 .

Lakini makundi ya wanaharakati wa mazingira wanasema mapendekezo hayo ni kawaida yangekuwa bora zaidi.

Katika kikao hicho hicho , kamati ya Muungano wa Ulaya imeiagiza Uingereza kuulipa Muungano wa Ulaya dola Bilioni mbili nukta saba .

Pesa hizo zimetolewa kufuatia mabadiliko ya utaratibu wa tume hiyo wa kuangalia viwango vya mafanikio ya kiuchumi ya nchi wanachama tangu mwaka 1995 .

Nchi za Uholanzi na Utaliano ni miongoni mwa nchi nyingine wanachama zinazokabiliwa na malipo ya ziada , huku Ujerumani na Ufaransa zikitarajia kupata punguzo la malipo kwa kulipa pesa taslim