Aomba kuoana ndani ya gari la polisi

Image caption Caine Hutchings akipendekeza kwa Emily Dukeson nia ya kutaka kuoana naye muda mfupi baada ya gari lake kugonga mti.Emily alikubali.

Caine Hutchings alipendekeza kwa Emily Dukeson nia ya kutaka kuoana naye muda mfupi baada ya gari lake kugonga mti.

Mwanamke alikubali pendekezo hilo la kuoana wakiwa katika gari la polisi wakifuatilia ajali ya barabarani.

Caine Hutchings alipendekeza kwa Emily Dukeson nia ya kutaka kuoana naye muda mfupi baada ya gari lake kugonga mti, wakielekea ufukweni mwa bahari ambapo awali alipanga kutoa pendekezo hilo.

Badala yake, wapenzi hao kutoka Radstock walikubaliana kufunga ndoa wakati wakiendeshwa kutoka eneo la tukio.

Hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa katika ajali ya Jumamosi karibu na Shapwick katika barabara ya A39 na hakuna faini iliyotozwa kutokana na ajali hiyo.

Bwana Hutchings, mwenye umri wa miaka 30, amesema: "Tulikuwa tu katika gari la polisi muda mfupi lakini ajali imefichua kila kitu, kwa hiyo niliamua kuwa nitatoa pendekezo langu hapo na kwa sababu lolote linaweza kubadili hali hiyo katika muda mfupi na sikutaka kusubiri zaidi. "Tulipiga picha ya mimi nikipiga goti moja chini mbele ya gari la polisi baada ya kwenda katika mkahawa au hakuna mtu anayeweza kuamini nilichofanya."

Bi Dukeson, mwenye umri wa miaka 27, amesema: "Sikuwa na wazo kwamba hilo litatokea. Lakini kwa namna ninavyofahamu tulikuwa tunakwenda Blue Anchor kuwachukua mbwa kwenda matembezini.

"Katika gari Caine aliuliza 'hivi kweli unafikiri tunakwenda mwendo wote huu ni kwa ajili ya kuwatembeza mbwa tu? na alivuta kikasha chenye pete.

PC Nicola Rickards, ambaye alikuwa akiendesha gari la polisi, alisema: "Ghafla alitoa kikasha katikati ya safari. Sina uhakika nani alifurahi zaidi."

Wapenzi hao wamesema walikuwa wanapanga kuoana mwaka ujao.