Balozi aifunda Yemen

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wapiganaji Yemen

Balozi wa Yemen nchini Uingereza UK, Abdulla Ali al-Rahdi ameiambia BBC kwamba nchi yake itageuka uwanja wa vita iwapo hatua ya usulhishi wa amani hautachukuliwa mapema.

Amesema kuwa machafuko hayo yakielendelea pia yataharibu uhusiano wa Yemen na nchi jirani na kuonekana ni eneo hatari katika suala la usalama.

Yemen imekuwa katika machafuko ya kisiasa tangu september pale waasi Wakishia kutoka kaskazini mwa nchi hiyo waliposhikilia eneo kubwa la mji mkuu wa nchi hiyo Sanaa

Hata hivyo vikosi vya serikali vilijaribu kukabiliana na waasi hao,lakini wapiganaji hao wa Sunni wanaoshirikiana na Al Qaeda wamekuwa wakiendesha mapigano makali huko Houthis.