24 wahofiwa kuaga dunia Zambia

Image caption mashua

Ripoti kutoka nchini Zambia zinasema kuwa wanafunzi 21 na walimu 3 wanahofiwa kuaga dunia baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kuzama kwenye ziwa Kariba.

Wote hao kutoka shule moja ya msingi walikuwa wakielekea kwenye shule moja ya upili kushiriki kwenye tamasha za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Zambia.

Taarifa kutoka kwa polisi zinasema kuwa huenda upepo mkali ulichangia kutokea kwa ajali hiyo.