Chelsea yaapa kuichapa Man United

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Chelsea/Man United

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa viongozi hao wa ligi ya Uingereza watajaribu kuimarisha mchezo wao dhidi ya Manchester United siku ya jumapili.

Mkufunzi huyo alichezesha kikosi kilichokuwa na mshambuliaji asiyejulikana wakati timu hizo mbili zilipotoka sare ya bila kwa bila msimu uliopita katika uwanja wa Old Trafford.

Lakini baada kushinda mechi 7 kati ya nane ,Mourinho amefurahishwa na mbinu anazotumia.

Chelsea imeanza vyema msimu huu hatua iliowafanya kuwa pointi kumi juu ya Manchester United ambayo imejikokota kuimarisha mchezo wake licha ya kununua wachezaji maarufu chini ya usimamizi wa kocha Louis Van Gaal.

Kocha huyo wa Uholanzi anatarajia kupunguza pengo kubwa la pointi kati yake na Mourinho ambaye alikuwa chini yake akisimamia kilabu ya Barcelona.