Nesi wa Ebola alalama alivyotengwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wauguzi

Muuguzi aliyetengwa aliporejea nchini Marekani baada ya kuwatibu wagonjwa wa ebola nchini Sierra Leone amelalamikia jinsi alivyohudumiwa.

Sheria mpya zilizotangazwa na majimbo matatu nchini Marekani yakiwemo New York , New Jersey na Illinois zinamaanisha kuwa kila mtu anayerejea kutoka nchi yoyote ya Afrika magharibi iliyoathirika na ugonjwa wa ebola, na huenda amekaribiana na wale walio na ugonjwa huo ni lazima awekwe kwenye karantini kwa muda wa wiki tatu

Kaci Hickox anasema kuwa hali aliyopitia ni ya kuogofia na huenda ikachangia wahudumu wengine wa afya kukosa kwenda Afrika magharibi kukabiliana na hali iliyopo.

Bi Hick OX ambaye alipatikana na maradhi hayo alisema kuwa alizuiwa kwenye uwanja wa ndege kwa muda wa saa saba.