Djokovic kiwango cha ubora charejea

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Novak Djokovic

Mcheza Tennis Novak Djokovic amesema kuwa hazingatii sana nafasi yake ya kwanza.

Amesema hayo wakati kiwango chake kikiwa kimerejea katika ubora baada ya kuwa baba kwa mara ya kwanza.

Mserbia huyo mwenye umri wa miaka 27, atacheza mechi yake ya kwanza siku ya Jumanne katika mashindano ya Paris Masters mchezo ambao unakuja ikiwa ni siku chache tu tokea mke wa mchezaji huyo Jelena Ristic kujifungua.

''nahisi kama tayari nimekuwa namba moja haswa baada ya kuwa baba wiki iliyopita'' alisema Djokovic.

Philipp Kohlschreiber ndiye mpinzani wake wa kwanza tangu apoteze mchezo wake kwa mchezaji anayeshika nafasi ya pili ya dunia Roger Federer huko mjini Shangai mwanzoni mwa mwezi huu.