Maelfu wakumbuka maandamano Hong Kong

Image caption Maelfu ya waandamanaji waadhimisha mwezi mmoja wa maandamano Hong Kong

Maelfu ya watu katika eneo la Hong Kong wamejitokeza katika maandamano nje ya makao makuu ya serikali kuadhimisha mwezi mmoja wa maandamano.

Wakifungua miavuli, ambayo inatumika kama alama ya maandamano, walikaa kimya kwa sekunde 87- ikiwa ni kumbukumbu ya mara 87 ambayo polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji.

Maandamano hayo yatashuhudia viongozi wa maandamano wakihutubia umati wa watu baadaye.

Wanaharakati wanataka demokrasia kamili Hong Kong.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maelfu ya waandamanaji Hong Kong wakiadhimisha mwezi mmoja wa maandamano.

Maandamano yanafanyika katika eneo ambalo lilishuhudia maelfu ya waandamanaji wakifurika mitaani baada ya polisi kufyatua gesi ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji wakati wa kilele cha maandamano hayo.

Waandamanaji walibeba mabango katika maandamano hayo. Bango lililokuwa mbele lilisomeka: "Nataka uchaguzi kamili"

Waandamanaji waliimba nyimbo kabla ya kukaa kimya kwa muda wa sekunde 87.

Wengine walicheza dansi kama sehemu ya maandamano.

Wiki iliyopita kwa mara ya kwanza viongozi wa maandamano na maafisa wa serikali wafanya mazungumzo, lakini hayakuwa na mafanikio katika kumaliza mgogoro huo.