Wakurdi wa Iraq kusaidia wenzao Syria

Haki miliki ya picha Getty
Image caption waziri mkuu wa Uturuki

Wapiganaji mia moja hamsini wa Kurdistan nchini Iraq wapo njiani kuungana na wakurdi wenzao katika mapigano dhidi ya wapiganaji wa Dola ya Kiilamu wa Islamic state nchini Syria.

Baada ya kuondoka katika ngome yao nchini Iraq, wapiganaji wa Peshmerga watasafiri kwa kupitia Uturuki kupitia Syria ili kuulinda mji wa Kobane.

Mashambulizi zaidi yameripotiwa kutoka katika eneo hilo Mwandishi wa BBC aliyekuwepo katika eneo la tukio aliona ndege za kivita zinazoongozwa na Majeshi ya Marekani zikizingira maeneo ya Dola ya kiilsam ya Islamic state.Uturuki imekubali kuruhusu idadi kamili ya wapiganaji vya Kurdi kupita nchini humo.

Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amesema Uturuki watawaruhus askari wa nchi kavu kupigana na wapiganaji wa jihad nchini Syria endapo majeshi washirika wa nchi za magharibi hayatafanya hivyo.