Scandnavia yaongoza, uwiano wa kijinsia

Image caption Wanawake walioshika nafasi za juu madarakani

Ripoti mpya iliyotolewa inaonesha kuwa nchi za SCANDNAVIA zinaongoza kwa uwiano wa kijinsia.

Katika ripoti yake ya mwaka iliyoitoa Jukwaa la kiuchumi duniani limeangalia fursa kwa wanawake katika nchi 142. Huku nchi za Afrika, zikiongozwa na Rwanda.

Miongoni mwa mambo yaliyozingatiwa katika ripoti hiyo, Kwanza, wanawake wanafanyakazi na kulipwa malipo sawa kwa kazi iliyosawa?. Je wananafasi ya kupata elimu?.

Maeneo mengine yaliyozingatiwa ni je wanawake wanaruhusiwa kushiriki katika masuala ya kisiasa haswa katika ngazi za juu, kuweza kushika nafasi za ubunge na hata madaraka ya juu zaidi. Nchi zilizotajwa katika ripoti hiyo kuongoza ni Iceland ikifuatiwa na Norway, Finland, Sweden, Denmark.

Phillipines nchi iliyo katika bara Asia imeshika nafasi ya tisa. Rwanda imeibuka kidedea kwa kuweza kuingia katika 10 bora ya nchi hizo 142, ambazo zilifanyiwa utafiti na pia kuwa nchi ya kwanza ya Afrika na zinazoendelea kuweza kushika nafasi ya kwanza katika ripoti hiyo.

Mafanikio ya Rwanda yanatokana na uwezo wa kupata huduma za afya na elimu, lakini pia, yanaangazia idadi kubwa ya wanawake wanaoshika nafasi za uwaziri.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mafanikio ya wanawake yanazidi kuonekana, kwani sasa kuna asilimia 26 zaidi ya wanawake wabunge duniani kote na asilimia 50 zaidi ya wanawake mawaziri kushinda ilivyokuwa miaka 10 iliyopita.

Utafiti huo uliofanywa umeonesha pia kuwa pengo kubwa katika usawa wa kijinsia lipo katika nchi za Chad, Pakistan na Yemen, ambako hakuna mabadiliko na mwaka uliopita.