Ban kuitembelea kambi ya Daadab

Haki miliki ya picha
Image caption Ban Ki Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatembelea kambi ya wakimbizi ya Daadab, nchini Kenya.

Hii ni mara ya kwanza kwa kingozi huyo mkubwa katika Umoja wa Mataifa kutembelea kambi hiyo kubwa ya wakimbizi.

Ban Ki Moon anatarajiwa kutathmini hali ya msongamano katika kambi hiyo na hali ya usalama ambayo imekuwa ikizorota mara kwa mara.

Aidha ripoti zinasema, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ataidhinisha kuondoka kwa baadhi wa wakimbizi wa kisomali waliojitolea kurudi nyumbani.