Boko Haram lakaribia mji wa Mabu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wasichana waliotekwa na Boko Haram

Ripoti kutoka nchini Nigeria zinasema kuwa watu wanaokisia kuwa wanamgambo wa Boko Haram wanaendelea kusonga mbele kwenda mji ulio kaskazini mashariki mwa nchi wa Mubi hata baada ya kutangazwa kuafikiwa makubaliano ya kusitisha vita.

Mji wa Mubi ulio karibu na mpaka na Cameron ndio mji wa pili kwa ukubwa kwenye jimbo la Adamawa.

Mkaazi mmoja aliiambia BBC kuwa wenyeji wa eneo hilo kwa sasa wanaukimbia mji wa Mubi.

Mpema mwezi huu serikali ya Nigeria ilitangaza usitishaji wa mapigano na Boko Haram kwenye makubaliano ambayo yangesababisha kuachiliwa kwa zaidi ya wasichana 200 wa shule waliotekwa nyara na kundi hilo.