Ukistaajabu ya Musa!

Haki miliki ya picha AFP
Image caption waliobahatika kuwa shule ndo hao, wengine huanza shule ya awali wakiwa na miaka 11.

Wakati harakati mbali mbali za kukabiliana na ndoa na mimba za utotoni zikiendelea na hasa katika nchi za Afrika, baadhi ya nchi barani humo zinakabiliwa na changamoto hiyo kupita kiasi.

Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Kesi ya kwanza na ya aina yake imefanyika na hukumu yake kutolewa nchini Ivory Coast baada ya mwanamume mmoja kumuoa binti yake wa umri wa miaka 11.

Kutokana na kitendo cha mwanamume huyo kumuoa binti yake alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na faini ya dola za Kimarekani mia saba.

Mwendesha mashtaka Rosine Kone amesema kwamba kesi hiyo ya aina yake itatuma ujumbe mzito kwa raia wa nchi hiyo ili wanaume waache tamaa.

Nao Umoja wa Mataifa unasema kwamba ndoa za utotoni nchini Ivory Coast si suala la kushangaza, kwani mmoja kati ya mabinti watatu huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka kumi na nane.