Ferrari na mtazamo mpya kibiashara

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Gari aina ya Ferrari

Mtengeneza magari ya kifahari ya michezo na mmilikiwa timu ya mbizo za magari ya Formula one ,ferrari,kampuni yake inatarajiwa kujitegemea kibiashara hii ikiwa ni mara ya kwanza tangu mnamo mwaka 1960.

Mmiliki wa sasa wa kampuni hiyo,Fiat Chrysler,amesema kwamba kampuni yake itauza hisa asilimia kumi ya biashara yake katika soko la hisa na kuzigawanya hisa zilizosalia miongoni mwa wawekezaji.

Fiat Chrystler anatarajiwa kukuza mtaji baada ya kuingiza dola za kimarekani elfu sitini ikiwa ni mpango wa ukuzaji mtaji ,na siku za hivi karibuni Ferrari ametengeneza faida kubwa kibiashara.