Michezo mchanganyiko

Haki miliki ya picha c
Image caption Furaha ya kombe

Baada ya mashabiki wa soka nchini Uingereza kukongwa nyoyo zao kwa kushuhudia mechi kadhaa za ligi kuu ya nchi hiyo mwishon mwa wiki, usiku wa kuamkia leo ilikuwa ni zamu ya kombe la ligi almaarufu kama CAPITAL ONE CUP. Timu kadhaa zilijitupa uwanjani ili kutafuta nafasi ya kuingia robo fainali yaligi hiyo.

Mkongwe Drogba ameweza kuisaidia Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mpambano dhidi ya Shrewsbury, Nae mtukutu Balotel akatia chachu katika ushindi wa mabao 2-1 iliyoupata Liverpool katik mchezo dhidi ya Swansea City.

Mashabiki wa Fulham huenda walilala mapema baada ya kushuhudia timu yao ikipokea kichapo cha magoli 5-2 pale walipoialika Derby. Bournemouth wakailaza West Brome kwa jumla ya mabao 2-1, huku Sheff Utd ikiibamiza MK Dons kwa ushindi wa mabao 2-1………..?

Nchini Urusi klabu ya soka ya CSKA Moscow imepunguziwa adhabu iliyopewa kutokana na vurugu zilizosababishwa na mashabiki wa timu hiyo mwezi uliopita katika mechi ya klabu bingwa barani ulaya ambayo timu hiyo ilipoteza dhidi ya AC Roma.

Timu hiyo ilitakiwa kucheza bila mashabiki mechi 3 za nyumbani za klabu bingwa Ulaya baada ya mfululizo wa matukio ya uovu ikiwemo matamshi ya kibaguzi.

UEFA imepunguza adhabu mpaka kufikia mechi 2 ambapo kati ya hizo ni ile ya wiki iliyopita ambayo iliishia kwa sare ya 2-2 dhidi ya Manchester City. Kupungua huku kwa adhabu kunatokana na rufaa iliyokatwa na timu hiyo japo adhabu ya kutouza tiketi katika mechi mbili za ugenini bado inaendelea.

Katika Tenis Novak Djokovic ambaye kwa sasa ni baba amemshinda Philipp Kohlschreiber katika shindano la Paris Masters.

Mserbia huyo ameshinda set 6-3 6-4 ikiwa ni siku 7 tu tokea mke wake Jelena kujifungua mtoto wao wa kwanza waliyempa jina la Stefan.

Djokovic sasa ni baba Stefan