Boko Haramu wazidi kuitesa Nigeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kundi la Boko Haram

Wakati kundi la kigaidi la Boko Haram likiukaribia mji mkuu wa Nigeria kwa upande wa kaskazini mashariki katika mji wa Mubi,ambako mapigano makali yameripotiwa eneo hilo pamoja na wito wa kusitisha mapigano kutolewa.

Wakati hayo yakijiri, Raisi wa Nchi hiyo Goodluck Jonathan amethibitisha kugombea muhula wa pili wa uraisi katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi February mwakani.

Goodluck anatarajiwa kuchukua fomu hii leo ya kugombea kuwa mgombea wa chama chake katika nafasi ya uraisi.ingawa yeye anawaza madaraka, serikali yake imekumbana na changamoto hata kupingwa kuhusina na namna inavyoshughulika na kundi la Boko Haram na vita wanavyoviendesha,na kushindwa kuwakomboa mabinti ya mia mbili wa shule ya Chibok walotekwa na kundi hilo m paka sasa.