Adhabu kali si dawa ya dawa za kulevya

Image caption Mwaka jana Uruguay ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuruhusu kilimo na matumizi ya mmea wa bhangi

Taarifa ya utafiti wa serikali ya Uingereza umeilinganisha nchi hiyo na nchi kama Ureno, ambako kukutwa na kiasi kidogo cha dawa za kulevya kunaadhibiwa vikali.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza wa chama cha Liberal Democrat Norman Baker amesema matokeo ya utafiti huo lazima umalize "mawazo yasiyo na maana" kuhusu dawa za kulevya kwa kuwa na mwelekeo mpya katika kutoa matibabu kwa watumiaji wa dawa hizo.

Serikali imesema haikuwa na lengo la kuhalalisha dawa hizo.

Ripoti hiyo imetolewa wakati wizara ya mambo ya ndani ikiweka sheria za kudhibiti ulevi.

Ripoti hiyo imeangalia njia mbalimbali zilizochukuliwa katika nchi 13 kukabiliana na dawa za kulevya zikilinganishwa na Uingereza.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Matumizi ya mmea wa Miraa au Mirungi ambao unasisimua mwili kwa mtumiaji unapigwa marufuku Uingereza kwa maelezo kuwa ni aina ya dawa za kulevya

Baada ya kupima njia hizo, kutoka ile ya kuvumilia kutowaona watumiaji wa dawa za kulevya kuwa wahalifu, utafiti huo ulihitimisha kuwa matumizi ya dawa za kulevya unachochewa na mambo mengi ambayo ni "magumu na yenye usumbufu kuliko sheria na usimamiaji wa sheria hizo pekee."

Hata hivyo, ripoti hiyo imebaini kuimarika kwa kiasi fulani afya za watumiaji wa dawa za kulevya nchini Ureno tangu mwaka 2001, wakati nchi hiyo ilipoona kuwa kutumia dawa za kulevya ni tatizo la afya zaidi kuliko kuwa uhalifu.

Wizara ya Mambo ya Ndani imesema matokeo haya hayawezi kuchangiwa pekee na hali ya kutowaona kuwa ni wahalifu watumiaji wa dawa hizi na serikali ya Uingereza kwa "hakika haina lengo la kuona dawa za kulevya kama si kosa la uhalifu."

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Mtumiaji wa dawa ya kulevya aina ya heroin akiandaa dawa hiyo tayari kwa matumizi

Bwana Baker amesema kuchukulia dawa za kulevya kama suala la kiafya kutasaidia zaidi kupunguza madhara ya dawa hizo.

Mapema mwaka huu, Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza Nick Clegg aliahidi kuondoa adhabu ya kifungo jela.

Bwana Clegg alimpa changamoto Waziri Mkuu David Cameron kuangalia masuala kama kutowatia katika hatia ya uhalifu watumiaji wa dawa za kulevya, japokuwa awali waziri mkuu alikataa wito wa Tume kufikiria suala hilo.

Danny Kushlick, mwanzilishi wa kikundi cha "Transform", ambacho kimekuwa kikipiga kampeni ya kurekebisha sheria kuhusu dawa za kulevya nchini Uingereza kwa miaka karibu 20 amesema ripoti hiyo ni hatua muhimu.

Amesema: "Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 40, wizara ya Mambo ya Ndani imekiri kuwa sheria kali dhidi ya dawa za kulevya si lazima kwamba zitapunguza viwango vya matumizi ya dawa za kulevya.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mkuu wa Wakala wa Kikosi cha Kulinda Mipaka ya Uingereza Brodie Clark akionyesha baadhi ya dawa za kulevya zilizokamatwa nchini Uingereza

"Kutoadhibiwa kwa kukutwa na dawa za kulevya hakuongezi viwango vya matumizi ya dawa hizo."

Sheria za dawa za kulevya katika baadhi ya sehemu duniani zimelegezwa katika miaka ya karibuni.

Mwaka jana, Uruguay ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuhalalilisha kilimo cha bangi pamoja na matumizi yake.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, jimbo la Colorado nchini Marekani lilikuwa la kwanza kuruhusu maduka kuuza bangi kwa sababu za kiraibu.