Vinasaba ni muhimu kupona Ebola

Haki miliki ya picha spl
Image caption Virusi vya Ebola

Vigezo vya kijenetiki vinaweza kuwa sababu muhimu kumwezesha mtu kunusurika na maambukizi ya virusi vya Ebola, wanasema wanasayansi wa Marekani.

Uchunguzi wa kisayansi uliofanyika kwa panya waliotungwa virusi walionyesha dalili tofauti kwa panya hao ambapo asilimia 19 walibaki bila kupata madhara ya virusi hivyo.

Hii inaweza kueleza kwa nini baadhi ya watu wanapona ugonjwa huu wakati wengine wakifa kwa maumivu, wamesema wanasayansi hao.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mfanyakazi wa afya akimhudumia mgonjwa wa Ebola

Uchunguzi wao umechapishwa katika jarida la Sayansi.

Wanasayansi kutoka vyuo vikuu vya Washington na North Carolina, na Taasisi ya Afya ya Taifa huko Montana, waliwapima panya ambao walitungwa virusi vya aina moja vya Ebola vinavyosababisha milipuko huko Afrika Magharibi.

Ingawaje panya wote walipoteza uzito katika siku chache za kwanza baada ya kupandikizwa virusi, karibu mmoja kati ya watano alipata nguvu na hakuonyesha kuwa na dalili za ugonjwa.

Lakini asilimia 70%ya panya walikuwa wagonjwa taabani, baadhi yao wakionyesha dalili za ini kushindwa kufanyakazi na kundi kubwa wakitokwa na damu ambayo ilichukua muda mrefu kuganda.

Image caption Kirusi cha Ebola

Pia panya hawa walikuwa na tatizo la damu kuvujia ndani, kuvimba bandama na kubadilika kwa rangi ya ini.

Pia walikuwa na uwezekano mkubwa wa zaidi ya asilimia 50% kufa kutokana na ugonjwa huo.

Angela Rasmussen, kutoka Maabara ya Katze katika chuo kikuu cha Washington, amesema namna tofauti za madhara ya maambukizi kwa panya hao inaonyesha aina ya dalili zilizooneka kwa binadamu wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mwaka 2014.

Watu walionusurika na ugonjwa wa Ebola hivi karibuni huenda wamekuwa na kinga dhidi ya virusi hivi au vinavyofanana, kinga ambayo imewaokoa.