Raia waandamana kupinga jeshi B.faso

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandamanaji nchini Burkina Faso.sasa wataka uongozi kupewa raia.

Waandamanaji wameanza kukusanyika kwenye mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougu kupinga hatua ya jeshi ya kutwaa uongozi wa nchi hiyo.

Vyama vya upinzani na mashirika ya umma vinataka uongozi wa kiraia wa kuongoza nchi hiyo hadi ufanyike uchaguzi mkuu wa kumchagua rais.

Wanasema kuwa usimamizi wa mabadiliko uko mikononi mwa watu na haustahili kunyakuliwa na jeshi.

Jana Jumamosi jeshi lilimteua Luteni Kanali Isaac Zida kama kiongozi wa serikali ya muda baada ya maamdamano yaliyofikisha kikomo uongozi wa rais Blaise Campaore.

Baada ya saa 24 za mvutano ndani ya jeshi kuhusu ni nani angeiongoza Burkina Faso, vyama vya kisiasa na mashirika ya umma vilitangaza ushindi kwenye maandamano yaliyomlazimisha rais Compaore kujiuzulu.

Marekani imeshutumu kile ambacho imekitaja kuwa jaribio la jeshi la kulazimisha matakwa yake kwa raia