Jeshi laombwa kurudisha mamlaka kwa raia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Barrack Obama ataka kurudishwa mamlaka kwa raia nchini Burkina Faso

Marekani imelaani kile ilichokitaja kuwa mipango ya jeshi nchini Burkina Faso ya kulazimisha inachotaka kwa watu raia kufuatia kujiuzulu kwa rais wa nchi hiyo Blaise Compaore.

Jeshi limemteua kanali Isaac Zida kama kiongozi mpya wa serikali ya mpito.

Lakini kwa upande wake Marekani inataka kuwepo utawala wa kiraia nchini Burkina Faso mbali na mipango ya kuwepo kwa uchaguzi wa urais, wito ambao pia ulitolewa na muungano wa Afrika.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kanali Issac Zida ambaye ameteuliwa na jeshi kuongoza serikali ya Mpito ya Burkina Faso.

Upinzani nchini Burkina Faso unasema kuwa hautakubali uongozi wa kijeshi na umeitisha maandamano leo Jumapili

Bwana Compaore ameikimbilia Ivory Coast baada ya kulazimishwa kuondoka madarakani kupitia maandamano.