Kombe la Dunia Tennis kuunguruma London

Haki miliki ya picha PA
Image caption Andy Murry

Fainali za dunia za tennis zitaanza kuunguruma mjini London juma lijalo ambapo bingwa mtetezi na mchezaji bora wa dunia Novak Djokovic wa Serbia amepangwa kuongoza kundi A pamoja na Stan Wawrinka wa Switzerland, mwenye kushika namba 4 kwa ubora duniani.

Bingwa wa Wimbledon 2013 muingereza Andy Murray ametupwa kwenye kundi moja na Mswiss Roger Federer kwenye kundi B litakalokuwa pia na Kei Nishikori wa Japan na Milos Raonic wa Canada. Washindi wawili kwa kila kundi watasonga mbele kwenye nusu fainali.

Murry mwenye miaka 27 ametwaa mataji matatu tofauti katika kipindi cha wiki sita tu zilizopita na kuingia fainali hizi za mwisho za mashindano za London. Ratiba hii imemtenganisha Murry na bingwa mtetezi Djokovic ambaye alimtwanga kwenye michezo Paris Masters wiki iliyopita na kumaliza mwendo wa ushindi wa mechi 11 mfululizo.