Watu 50 wauawa Pakistan

Image caption wapiganaji wa Taliban

Zaidi ya watu 50 wameuawa na wengine 100 kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu la kujitoa muhanga huko Pakistan karibu na mpaka wan chi hiyo na India.

Mlipuko huo ulitokea karibu na kizuizi cha mpakani cha Wagah karibu na eneo kupita mpaka wa kuelekea Lahore. Hata hivyo kati ya raia hao waliojeruhiwa 15 hali zao ni mbaya,na kwamba wafanyakazi wa idara ya usalama katika mpaka wa Pakistan wamefariki dunia. Mlipuko huo ulitokea majira ya jioni wakati wa sherehe za ushushaji bendera katika mpaka wa Wagah Kundi la wapiganaji wa Taliban wamekiri kushiriki katika tukio hilo. Waziri mkuu wa India Narendra Modi ameelezea shambulio hilo kwamba moja kati ya matendo yakusikitisha ya kigaidi na ambacho kina madhar kwa raia na taifa katika sektaya utalii.