Liverpool mdomoni mwa Madrid leo

Haki miliki ya picha AP
Image caption Madrid vs Liverpool

Michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya inaingia mzunguko wa pili hii leo kwa mechi za marudiano ambapo mabingwa watetezi Real Madrid watakuwa nyumbani Santiago Bernabeu kukipiga na Liverpool..ambayo katika mechi ya awali ilikubali kichapo cha fedheha nyumbani Anfield.

Kocha wa Liverpool Brendan Rogers amesema hatomchezesha mshambuliaji wake Daniel Sturridge licha ya kusafiri naye hadi mjini Madrid kwa madai kuwa bado hajawa sawa kukabiliana na mechi kama hiyo…huku mwenzie wa Madrid Carlo Anceloti akisema leo anamrudisha kiwanjani Gareth Bale baada ya kuwa nje ya uwanja kutokana na kuwa majeruhi kwa mwezi mzima. Kwengineko Zenit St Petersburg ya Urusi itamenyana na Bayer Liverkusen ya Ujerumani, Arsenal itakuwa nyumbani Emerates wakiwakaribisha Anderletch ya Ubelgiji ilhali Juventus ya Italia wakikiputa na Olympiakos ya Ugiriki. Hapo kesho Manchester City watakwaruzana na CSKA Moscow ya Urusi dimbani Etihad,FC Bayen Munchen watachuana na AS Roma…wakati ambapo Ajax Amsterdam watapambana na FC Barcelona..na Paris St Germain watacheza na Apoel Nicosia.