Afganistani kupambana na Ubakaji

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wanawake nchini Afghanistan

Serikali nchini Afganistani inachukua hatua ya kukabiliana na kundi linadaiwa kuhusika na ubakaji, baada ya mume wa muhanga wa tukio la ubakaji (Jahangir) kutoa hisia zake kupitia televisheni huku akidai haki.

Mke wa (zeba) anasema alibakwa miaka mitano iliyopita na wanaume nane katika jimbo la Badakhshan wakati akiwa nyumbani na watoto wake.

Wanaume wawili wanashikiliwa na polisi, pia serikali yaagiza watu sita wengine kukamatwa kutoakana na kesi ya ubakaji.

Familia ya muhanga huyo inasema wahusika wa tukio hilo wanammalaka makubwa kisiasa,wanasema wamepokea vitisho vya kuuliwa endapo watajaribu kuiendeleza kesi hiyo.