Burkina Faso:Marais 3 kuzuru nchini humo

Image caption Viongozi wa kijeshi waliochukua mamlaka nchini Burkina Faso

Marais wa Ghana, Nigeria na Senegal wanatarajiwa kuzuru Burkina Faso hii leo kushinikiza viongozi wa kijeshi nchini humo kurejesha utawala wa kiraia.

Kiongozi wa mpito luteni kanali Isaac Zida, amesema kuwa atarejesha mamlaka katika kipindi cha wiki mbili, muda uliotolewa na Muungano wa Afrika.

Ameahidi kuunda serikali ya umoja na hivyo kuepuka uwezekano wa kuwekewa vikwazo.

Viongozi wa upinzani bado hawajabainisha nafasi ya jeshi katika kipindi cha mpito.

Jeshi lilichukua udhibiti wa nchi baada ya maandamano ya ghasia kulazimisha kujiuzulu kwa aliyekuwa rais Blaise Compaore aliyeongoza nchi hiyo miaka 27