Wanajeshi wa Libya wafukuzwa Uingereza

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wa Libya

Wanajeshi kutoka nchini Libya wamerejeshwa nchini kwao kutokana na kukosa uadilifu wakiwa mafunzoni Uingereza huku wengine wakituhumiwa kufanya vitendo vya ukatili wa kimapenzi.

Wanajeshi hao waliokuwa mafunzoni nchini Uingereza, 300 kati yao wamesharejeshwa Libya kutokana na tuhuma kuhusiana na unyanyasaji wa kimapenzi.

Waziri wa Ulinzi wa Libya amethibitisha kurejeshwa kwa askari hao na kuongeza kuwa wengine watarejeshwa siku chache zijazo.

wanajeshi wawili wa Libya wamekiri kufanya vitendo vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake huko Cambridge, ambapo wawili wameshafikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashitaka ya ubakaji.

Baadhi ya wakazi wa eneo jirani na kambi ya jeshi walipo wanajeshi hao wa Libya,wamesema kuwa wamekuwa wakiwaona wanatoka nje ya ngome za jeshi kwaajili ya kununua pombe, na tayari waziri wa ulinzi amekiri kupokea mashtaka hayo na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wanajeshi hao wa kigeni.

Waziri Libya amesema wanajeshi hao wanaruhusiwa kutoka nje ya kambi kwa saa tatu wiki kwani ameongeza kuwa madhara ya askari hao kuzagaa mitaani ni makubwa na wengine hujitumbukiza katika matumizi dawa za kulevya na ulevu wa kupindukia.