Ushindi wa Republican:Obama aita kikao

Haki miliki ya picha AP
Image caption rais Obama akiwa katika ikulu ya whitehouse

Baada ya kushindwa vibaya kwa chama cha Democrat kwenye uchaguzi wa viti vya bunge la seneti nchini marekani rais wa marekani Barack Obama amewakaribisha viongozi wa baraza la congress kutoka vyama vyote katika ikulu ya white White House siku ya ijumaa kujadili mwelekeo wa siasa za nchi hiyo.

Kutoweza kufanya kazi kwa pamoja baina ya rais na Congress kumezorotesha kupitishwa kwa miswada na viongozi wa Republican.

Seneta wa Republican na kiongozi wa walio wengi Mitch Mc Connell amepata tena kiti chake katika jimbo la Kentucky.

Chama cha Republican kimezoa viti vingi katika uchaguzi huo na kukifanya kuchukua udhibiti wa taasisi hizo muhimu dhidi ya kile cha Democrat.

Kiongozi wa zamani wa seneti kutoka chama cha Democratic , Harry Reid, amemuita Mitch McConnell kumpongeza na akasema ilikuwa ni wazi kwamba wapiga kura walitaka vyama vyote kushirikiana.

Mwenyekiti wa Kamati ya kitaifa ya Republican Reince Priebus amesema kuwa umma wa wamarekani umekiamini chama chake.