Burkina Faso kufanya uchaguzi mkuu 2015

Image caption Luten Kanal Isaac Zida

Vyama vya siasa nchini Burkina Faso vimekubaliana kuwa na uchaguzi mkuu mwezi Novemba 2015 ikiwa ni harakati za kurejesha utawala wa kiraia na demokrasia..

Hata hivyo mazungumzo hayo yameisha bila kuwa na ufumbuzi kuhusiana na nani atakayekuwa kiongozi wa mpito hadi kufikia muda wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kufuatia kuangushwa kwa aliyekuwa raisi wa taifa hilo la Afrika Magharibi Blaise Compaore.

Jeshi la nchi hiyo limekuwa likishikilia madaraka ya tangu aondolewe madarakani kutokana na maandamano ya raia waliokuwa wakishinikiza Rais Compaore.

Umoja wa Afrika jumatatu wiki hii umetoa muda wa wiki moja kufanyika kwa mabadiliko ya utawala na kukabidhiwa kwa wananchi na siyo jeshi tena.

Luten Kanal Isaac Zida ambaye ni kiongozi wa mpito wa kijeshi ameahidi kufuata ushauri huo wa umoja wa Afrika kwa kukabidhi madaraka kwa wananchi ndani ya muda huo wa wiki mbili.