Mitandao yatumiwa kushambulia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mitandao ya mawasiliano inadaiwa kutumiwa vibaya kudhuru wengine.

Christopher Todd amekiri kuwatuma picha ya kudhalilisha wazazi wa mpenzi wake wa zamani.

Kijana mmoja ambaye aliachwa na mpenzi wake, baada ya kugunduliwa kutokuwa muaminifu katika mahusiano yao, amezua mtafaruku na kusababisha kupewa hukumu baada ya kutuma ujumbe wa simu kwa wazazi wa msichana, wenye kuonesha picha za utupu za mpezi wake huyo wa zamani kama hatua ya kulipiza kisasi.

Christopher Todd amekiri kuwatuma picha wazazi wa Hannah Davison kwa njia ya ujumbe wa simu.

Todd aliachwa na mpenzi wake huyo, baada ya kufumaniwa na mwanamke mwingine.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 21, aliishiwa nguvu baada ya kujua kwamba ujumbe huo wenye picha yake ya utupu, ulifunguliwa na baba yake mzazi.

Todd amehukumiwa na mahakama ya Tyneside kusini, nchini Uingereza, baada ya kukutwa na kosa la kutuma ujumbe uliomdhuru na kumdhalilisha mwenzie, ambao pia ulikuwa ukidai kwamba Hannah amekuwa akisambaza magonjwa ya kuambukiza.

Todd alikuwa na tabia ya kumtukana mpenzi wake huyo wa zamani kila anapolewa pombe na kwamba ujumbe huo wa mwisho alimtumia mama yake Hannah, baada ya kuona mpenzi wake huyo hamjibu, lakini bahati mbaya baba yake msichana huyo alifungua na kuusoma.