Burkina Faso:Jeshi lapuuza wito wa AU

Image caption Kiongozi wa mpito wa Burkina Faso, Isaac Zida

Kiongozi wa mpito wa Burkina Faso ametupilia mbali muda wa wiki mbili wa kukabidhi madaraka uliotolewa na Umoja wa Afrika wa kukabidhi madaraka kwa Raia.

Luteni Kanali Isaac Zida amesema hawaogopi vikwazo , na kuwa wanajali zaidi kuhusu uimara wa nchi yao.

Zida alifanya mazungumzo na upinzani na asasi za kiraia na kukubaliana kuitisha uchaguzi mwakani.

Jeshi lilishika madaraka baada ya kifo cha Rais Blaise Compaore ambaye alishinikizwa kujiuzulu baada ya kutokea maandamano wiki iliyopita.