Rais aistisha ziara zake

Haki miliki ya picha AFP Getty
Image caption Ndugu na jamaa wa wanafunzi walopotea

Rais wa Mexico,Enrique Pena Nieto, amesema kwamba atasitisha ziara zake za kimataifa zijazo,ili kushughulikia suala linalotatiza na lenye kukua siku hadi siku la kutoweka kwa wanafunzi arobaini na watatu .Maandamano yameibuka tena katika miji kadhaa mapema wiki hii,waandamanaji wakitoa wito wa suala hilo kupewa uzito unaostahili.

Wanafunzi hao walitoweka baada ya mapambano na polisi upande wa kusini magharibi mwa mji wa Iguala mnmo mwezi September.Crisoforo Garcia Rodriguez ,ndiye aliyeanzisha harakati za kuwasaka wanafunzi hao katika maeneo wanamoishi.

Naye akasema kwamba wametafuta miili ya wanafunzi hao kwa siku kadhaa na wakagundua makaburi ya jumla yapatayo 26.wakatoa taarifa polisi.walipofukua wakakuta mifupa ambayo haihusiani na wanafunzi hao,japokuwa ni mifupa, haiondoi heshima ya binaadamu ,lakini tunao ushahidi mwingine tuliougundua, vipande vya mavazi,mabegi ya mgongoni ya wasichana ,vitambulisho,kadi za benki vilivyochomwa moto.