Obama sasa atafuta usaidizi wa Iran

Image caption KIongozi wa dini nchini Iran Ali Khamenei na rais Obama kulia

Gazeti la Marekani limeripoti kuwa rais Obama alimuandikia barua ya siri kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, kujadili uwezekano wa ushirikiani dhidi ya Wanamgambo wa Islamic State .

Gazeti hilo la The Wall Street Journal limesema Bwana Obama alituma barua hiyo mwezi uliopita ambayo kichwa chake kilikuwa "maslahi ya pamoja" katika kupigana na wanamgambo wa IS ndani ya Iraq na Syria.

Lakini rais Obama alisisitiza kuwa ushirikiano wowote utatarajia kukubali kwa Iran kupunguza kiwango chake cha mpango wa nuklia.

Duru za Iran zimeithibitishia BBC kuwa Bwna Khamenei alipokea barua kutoka kwa Obama ,lakini msemaji wa ikulu ya White house amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa sera ya Marekani kwa Iran haijabadilika