Umri wamvua Miss Tanzania taji

Huwezi kusikiliza tena

Miss Tanzania Sitti Mtemvu amejivua taji la Miss Tanzania aliloshinda mwaka huu mjini Dar es Salaam baada ya kuzongwa na mashabiki kuhusu umri wake.

Akizungumza na BBC Mkurugenzi wa Lino International Agency Hashim Lundenga waandaji wa shindano la Miss Tanzania amesema kuwa mrembo huyo amejivua mwenyewe taji hilo kwa kuandika barua bila kushinikizwa na mtu yeyote.

Tangu atangazwe mshindi kumekua na malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu wakimtuhumu kuwa alidangaya umri wake ili atimize vigezo vya kushiriki shindano hilo.

Pia Sitti alituhumiwa kuwa ana mtoto jambo ambalo pamoja na shutuma zingine alikanusha mbele ya waandishi wa habari mjini Dar es Salaam.

Kamati hiyo imemtangaza Lilian Kamazima ambaye ni mshindi namba mbili wa Miss Tanzania