Tuzo ya BBC ya mchezaji bora Afrika 2014

Image caption Tuzo ya BBC ya mchezaji bora Afrika mwaka wa 2014 imetangazwa

Orodha ya wachezaji tano wanaowania tuzo ya BBC ya mchezaji bora Afrika mwaka wa 2014 imetangazwa.

Bingwa mtetezi,Yaya Toure ametajwa kati ya watano hao kwa mara ya sita mfululizo pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang, Yacine Brahimi, Vincent Enyeama na Gervinho.

Image caption Vincent Enyeama

Mshindi atachaguliwa na mashabiki wa mpira kote barani Afrika hadi Novemba tarehe 24

Unaweza kupiga kura yako kupitia kwenye mtandao huu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Gervinho

Au piga kura yako kwa tuzo ya BBC ya mchezaji bora wa Afrika mwaka wa 2014 ukitumia ujumbe mfupi .

Ada ya kimataifa itatozwa.

Sheria na masharti kutumika.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Yacine Brahimi

Mshindi atatangazwa jumatatu tarehe mosi Desemba.

Wanne kati ya wachezaji wanaowania tuzo hii walishiriki kombe la dunia huko Brazil.

Mwaka huu itakumbukwa ilikuwa ni historia kwa mataifa mawili ya Afrika kufuzu katika mkondo wa maondoano wa kombe la dunia.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Yaya Toure

Mlinda lango Enyeama alishiriki katika mkondo wa 16 bora na timu ya Nigeria, naye Brahimi alifuzu katika hatua hiyohiyo na Algeria.

Enyeama, 32, alitua Brazil baada ya kushamiri kati klabu ya Lille huko Ufaransa ambapo alikuwa hajafungwa bao lolote katika mechi 21 msimu uliopita.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pierre-Emerick Aubameyang

Huko Uhispania juhudi za mshambulizi Brahimi akihudumia kandarasi yake katika klabu ya Granada ilimpelekea kutuzwa kama mchezaji bora kutoka Afrika nchini humo mbali na kuandikisha mkataba wa kudumu na klabu ya Porto.

Wawili hao wamechangia pakubwa katika ufanisi wa vilabu vyao .

Mchezaji mwengine aliyeonyesha udedea wake ni mshambulizi wa Ivory Coast Gervinho.

Mshambulizi huyo wa Roma ya Italia ametulia tangu awasili kutoka klabu ya Arsenal, tayari amefunga mabao 10 katika mechi 39 za ligi kuu ya Italia Serie A .

Yeye na Mchezaji mwenza wa The Elephants ya Ivory Coast Yaya Toure hakutamba huko Brazil lakini wameshamiri katika ligi za vilabu.

Toure ambaye mapema msimu huu alihitilafiana na klabu ya Manchester City hata baada ya kuisadia kunyakua taji lao la pili la ligi ya Uingereza katika kipindi cha miaka mitatu. Man city pia ilitwaa taji la Capital One.

Mchezaji mwengine ambaye ametajwa katika tano bora ni Aubameyang

Licha ya kuwa hakukuwa Brazil katika kombe la dunia kwa sababu taifa lake la Gabon halikufuzu mchezaji huyo wa Borussia Dortmund ametajwa katika kikosi hicho kwa mwaka wa pili mtawaliwa. Kiungo huyo ambaye amekuwa Ujerumani kwa msimu wa pili amefunga mabao matatu katika ligi ya mabingwa barani Ulaya tayari.

Washindi wa zamani wa tuzo ya mchezaji bora ya BBC :

2013 - Yaya Toure (Ivory Coast Na Manchester City)

2012 - Chris Katongo (Zambia Na Chinese Construction)

2011 - Andre 'Dede' Ayew (Marseille Na Ghana)

2010 - Asamoah Gyan (Sunderland Na Ghana)

2009 - Didier Drogba (Chelsea Na Ivory Coast)

2008 - Mohamed Aboutrika (Al Ahly Na Misri)

2007 - Emmanuel Adebayor (Arsenal NaTogo)

2006 - Michael Essien (Chelsea Na Ghana)

2005 - Mohamed Barakat (Al Ahly Na Misri)

2004 - Jay Jay Okocha (Bolton Na Nigeria)

2003 - Jay Jay Okocha (Bolton Na Nigeria)

2002 - El Hadji Diouf (Liverpool Na Senegal)

2001 - Sammy Kuffour (Bayern Munich Na Ghana)

2000 - Patrick Mboma (Parma Na Cameroon)