Roger Federer aanza vyema katika Tennesi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption furaha ya ushindi ya Roger Federer

Bingwa wa dunia katika mchezo wa Tennesi Roger Federer ameanza vyema safari yake na kushika nafasi ya saba mwishoni mwa msimu baada ya kumshinda mpinzani wake mkanada Milos Raonis mjini London.

Federer anaungana na mjapani Kei Nishikori kileleni mwa kundi B baada ya mjapani huyo kumpiku Andy Murray.

Kipindi cha pili cha mchezo huo mwanzoni mwa wiki hii itamshuhudia Federer akipimana ubavu na Nishikori naye Murray atakuwa kwenye kibarua kingine atakapokuwa katika piga nikupige na Mcanada Raonic.

Federer atakuwa kibarua kigumu cha kutaka kuufunga mwaka huu kwa kubaki namba moja duniani katika mchezo huo lakini hayo atayathibitisha katika nusu fainali haraka iwezekanavyo.

Federer ameanza vyema kwa mshusha Raonic katika nafasi ya kwanza katika seti za awali na kipindi cha pili walitunishiana msuli vilivyo katika muda wa saa moja na dakika ishirini na nane.

Ukafika wakati wa kujinasibu alipokuwa akiongea na waandishi habari na alisikika akisema, nilikuwa na furaha kwa jinsi nilivyocheza,na kisha kuwaambia umati nashukuru sana kwa mapokezi nlipoingia humu ndani .

Na kisha alikiri kwamba kipindi cha pili hakikuwa rahisi kwake,kilikuwa mtihani kizito na ilikuwa ni seti muhimu kushinda.mpinzani wangu hakucheza vizuri hivyoo,ili ilkuwa lazima ushindi,nafuu kidogo, kundi letu si mchezo, kadiri unavyoshinda ndivyo ushindani unavyoongezeka zaidi, na ndivyo ninanvyomkaribia Nishikori, nitakwaana naye.