Nani mwenyeji CAF 2015?

Haki miliki ya picha caf
Image caption Kombe la mataifa ya Africa

Hatma ya nani atakuwa mwenyeji wa kombe la mataifa ya Africa 2015 maarufu kama Africa Cup of Nations lazima ajulikane, kwani kamati ya shirikisho la vilabu vya soka barani Africa imekutana kujadili juu ya suala hili .

Morocco ndiye aliyekuwa anapewa nafasi kubwa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kuanzia tarehe 17 mwezi wa kwanza hadi mwezi wa pili tarehe 8, lakini kuna kila dalili Morocco inataka kuahirisha michuano hiyo kwa hofu dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola kuwa utaingia nchini humo.

Leo ndiyo leo, leo inapaswa kuwa siku ya kuamua kati ya Morocco na bodi ya shirikisho la mpira wa miguu barani Africa CAF, ile sintofahamu baina yao inatatuliwa.

Mwishoni mwa wiki iliyopita waziri wa michezo wa Morocco,alisimama na kuongea kwa kifupi yakwamba hawataweza kuwa mwenyeji wa michuano hiyo na badala yake wasikilizwe ombi lao la kuahirishwa kwa michuano hiyo mpaka mwaka wa 2016.

Wakati hayo yakijiri CAF wametoa msimamo wao ya kuwa tarehe ya kuanza kwa michuano hiyo haitabadilika,sasa swali linakuja je CAF wana nchi nyingine iliyotayari kupokea michuano hiyo na kuwa mwenyeji? Ilhali imebakia wiki kumi tu? Na kama inawezekana basi itakuwa ni kati ya nchi zilizokuwa wenyeji wa michuano hiyo miaka ya karibuni,ambayo CAF ina uhakika na miundo mbinu yake na uwanja ulio tayari ndani yake.

Mnamo mwaka 2013, mwenyeji wa michuano hiyo ilikuwa ni Africa Kusini ambayo tayari imekwishatoa msimamo wake kuwa wala wasiitie mawazoni kuwa wao ndo kimbilio la kunusuru michuano ya mwaka huu.

Nao CAF sasa wanatarajiwa kutoa tamko lao la mwisho juu ya suala hili, haraka iwezekanavyo .