Viongozi wa China na Japan wakutana

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Viongozi hawa wamekutana kwa mara ya kwanza tangu waingie mamlakani

Rais wa Uchina, Xi Jinping na waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe wamefanya mazungumzo kwa mara ya kwanza tangu wote washike madaraka.

Mkutano wao unaonekana kama hatua ya ufanisis ya juhudi za kutatua taharuki iliyokuwepo kati ya nchi hizo kutokana na madai ya Japan kuthibiti visiwa katika bahari ya kaskazini mwa Uchina.

Baada ya dakika thelathini za mazungumzo Bwana Abe aliondoka na kusema kuwa hiyo ndiyo hatua ya kwanza ya kuboresha mahusiano.

Mkutano huo ulifanyika Beijing wakati viongozi kutoka katika maeneo ya Asia walikutana katika kongomano la kibiashara la APEC.