India:Wanafunzi wahalalisha udanganyifu

Haki miliki ya picha
Image caption Wanafunzi wenye nacho wamekua wakitoa hongo kufaulu masomo

Mara nyingi wanafunzi wako makini katika kuhakikisha wanapata haki zao, lakini hivi sasa mambo yamekua tofauti, baadhi yao wanazungumzia haki ya kufanya udanganyifu kwenye mitihani ya Chuo kikuu.

Mmoja wa wanafunzi Pratap Singh kutoka jimbo la Uttar Pradesh amesema kuwa udanganyifu ni haki yao ya kuzaliwa.

Rushwa wakati wa mitihani ni jambo la kawaida katika eneo hilo, walio na pesa huhonga ili kufanikiwa kwenye mitihani.isitoshe kuna kundi la vijana ambao ni madalali wanaowaunganisha wanafunzi wanaotaka kufaulu na uongozi unaohusika na maswala ya mitihani.

Pia kuna tabaka la wanafunzi ambao wanafahamika vizuri kwa kuwa na uhusiano na maswala ya kisiasa,wasimamizi wa mitihani hawathubutu kuwagusa

hivyo basi kama wenye pesa na wenye kujulikana kisiasa wanaweza kulaghai kwenye chumba cha mtihani, Wanafunzi masikini wanauliza kwa nini wao wasifanye hivyo.