Je wanaume watasusia ngono Kenya?

Image caption Kiongozi wa shirika la maendeloe la wanaume Kenya Nderitu Njoka (kushoto) na wanaume wenzake

Wanaume nchini Kenya wameelezea hisia mseto kuhusu wito wa kiongozi wa shirika la maendeleo la wanaume nchini humo kwamba hii leo wasusie tendo la ndoa na kuonyesha hisia za mapenzi kwa wanawake.

Wiki jana kiongozi huyo Nderitu Njoka amewataka wanaume nchini Kenya kufanya hivyo kuadhimisha siku ya kimataifa ya uhuru kwa wanaume inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 11 mwezi Novemba.

Bwana Nderitu amewataka wanaume wote kutojihusisha na wanawake kimwili , wawe wameoa au la kama ishara ya kuonyesha ghadhabu yao kwa ongezeko la dhuluma wanazotendewa wanaume pamoja na ongezeko la utumiaji wa dawa za kulevya na pombe miongoni mwa wanawake.

Image caption Bwana Njoka amewataka wanaume kususia vitendo vya mapenzi kama njia ya kulaani dhuluma dhidi ya wanaume

Wito huo hata hivyo umepuuzwa na baadhi ya wanaume ukitajwa kuwa njama ya bwana Nderitu kujipa umaarufu katika vyombo vya habari.

Hatua hiyo pia inatumiwa kjuonyesha kero la wanaume kutokana na hatua ya serikali kutenga shilingi bilioni mbili kwa mahitaji ya wasichana wakati ikikosa kutoa mchango kama huo katika kusadia wanaume wengi kufanyiwa tohara.

Njoka alinukuliwa akisema kuwa kidini wanaume ndio viongozi wa familia lakini leo wamedhalilishwa huku wanawake wakitawala dunia.