Soko la Nywele bandia lashamiri China

Image caption Nywele bandia ambazo wanawake wanapenda kuvaa siku hizi.

Nchini China nywele za bandia ni biashara kubwa sana , wanunuaji katika maduka ya urembo na saluni huambiwa kuwa nywele hizo ni za kweli, lakini ukiziangalia kwa karibu zaidi, wakati mwingine hazionekani hivyo.

Katika kiiji kimoja, jimbo la Hunan, katikati ya China,Katika mitaa ya kijiji hicho inaonekana kuwa na nywele hizo , baadhi ya nywele hizo ni za kweli lakini nyingine si nywele za binaadamu isipokua manyoya ya mbuzi.

Mtu mmoja anafanya kazi ya kukusanya nywele, anasema anapogonga kengele wanawake hutoka kisha mtu huyo huwakata nywele kwa ajili ya kuuza.Mwenyewe anasema anawapa hela nzuri.

Image caption Nywele za bandia zinazoelezwa kuwa za binadamu huchanganywa na manyoya ya mbuzi bila mteja kujua

Baada ya kukusanya nywele,huzipeleka kwenye kiwanda kidogo ambacho kuna wanawake ambao huzitengeneza na kuwa nywele za bandia.

Nikitazama ninaona baadhi ya nywele zinazosukwa pamoja ni za binaadamu lakini nyingine sio kabisa, na mtu huyu huuza nywele hizo kwa viwanda vikubwa ambapo huwekwa dawa za kemikali kabla ya kuuzwwa madukani na nchi nzima.

Nywele hizo hufikishwa mpaka mjini Guazngzhou,mji ulio maarufu kwa shughuli za biashara.

Katika eneo hilo hakuna mteja wa asili ya kichina wanunuaji wengi wanatoka Afrika , Nigeria, Ghana,Congo, Afrika kusini,Angola na Uganda