'Moyo wangu ulisimama kwa dakika 45'

Image caption Moyo wa Ruby Graupera uliancha kudunda kwa dakika 45 ingawa baadaye alipata fahamu

Kwa namna alivyoonekana tu Ruby Graupera Cassimiro alikua amepoteza maisha.

Moyo wake uliacha kupiga kwa dakika 45, madaktari waliokuwa wakimfanyia upasuaji kumzalisha mtoto, waliwakusanya wanafamilia kwa ajili ya kusema buriani.

Kilichofuata hapo baadae mapigo ya moyo yakaanza tena kurudi na kuonesha kwenye kifaa maalum mithili ya kompyuta

Graupera Cassimiro alikua hai.Daktari Jordan Kanurr ameonyesha kushangazwa na tukio hilo wala pia hakuwahi kusikia kwa Madaktari aliokuwa akifanya nao kazi.

Mama huyu mwenye umri wa miaka 40, ambaye alijifungua mtoto wake akiwa na afya njema amewashtua sana madaktari.

''Nilikuwa nimekufa,'' Ruby aliambia kituo cha habari cha ABC . ''Mume wangu aliniambia niligeuka rangi mithili ya majivu.Mwili wangu ukawa baridi sana na kwamba mdomo wangu ulikuwa umekauka na hata kukosa rangi. ''

Image caption Ruby Graupera ametajwa kama mwanamke wa miujiza baada ya moyo wake kusimama kwa dakika 45

Baadaye Ruby alibandikwa jina na kuitwa mwanamke wa muujiza, ambaye moyo wake ulisimama kwa dakika 45 lakini akaanza tena kupumua.

Graupera alipata tatizo ambalo huwa ni nadra sana kushuhudiwa. Maji yanayomzunguka mtoto tumboni yalichanganyika na mzunguko wa damu wa mama na kusababisha moyo kukandamizwa hali iliyofanya mzunguko wa damu kusimama.

Alichokumbuka cha mwisho kabla ya moyo wake kusimama ni pale alipopelekwa hospitalini kwa kiti cha magurudumu na anasema kilichofuata, alilala usingizi mnono.

Baadaye Ruby aliacha kupumua. Madaktari walijaribu kumuamusha hata kwa kutumia mashine bila mafanikio. Moyo wake ulisimama kwa dakika 45.

Madaktari wanasema yaliyomkuta mzazi huyu ni miujiza mikubwa kwa kuwa hajapata madhara yoyote kwenye ubongo ingawa mapigo ya moyo yalisimama kwa muda mrefu.