Wanasayansi wajawa na shauku ya kimondo

Haki miliki ya picha Getty

Wanasanyansi wa safari za anga za mbali wamejawa na shauku ya kutaka thibitisho kwamba Chombo kilichopelekwa na kutua kwenye kimondo au nyota mkia yaani Comet iliyo umbali wa zaidi ya kilometa nusu bilioni kutoka duniani.

Hapo jana Chombo hicho kiliwezesha kuwekwa kwa historia ya kuwa kifaa cha kwanza kuwahi kutengenezwa na binadamu kutua kwenye kimondo, kazi iliyochukua zaidi ya miaka 10.

Hata hivyo huenda bado kifaa hicho hakijajibanza kwenye kimondo hicho chenye upana wa kilometa mbili , kama ilivyotarajiwa-Data mpya na hasa picha zinasubiriwa kwa hamu kubwa.