Mwanamke mzazi abakwa hospitalini.

Haki miliki ya picha British Broadcasting Corporation
Image caption Mwanamke nchini Pakistan

Polisi nchini Pakistan wanawashikilia wanaume watatu kwa kosa la utumizi dawa za kulevya na ubakaji kwa mgonjwa aliyefuata matibabu katika hospitali ya serikali.

Mwanamke huyo, ambaye alijifungua hivi karibuni,alikwenda katika eneo la Burewala Mashariki ya jimbo la Punjab,iliko hospitali hiyo na alikwenda hapo akiwa na mumewe pamoja na mtoto wao mchanga kwa uchunguzi wa kitabibu.

Mume wa mwanamke huyo alimwacha mkewe kitambo kifupi tu na aliporejea eneo alipokuwa ,hakumkuta ila mtoto na begi la mwanamke huyo vimetelekezwa.

Saa kadhaa baadaye,alimpata mkewe akiwa amelala katika chumba chenye kiza ,kilichomo katika hospitali hiyo na kuthibitika kuwa amebakwa .

baada ya fahamu kumrejea mwanamke huyo alisema kwanza alichomwa sindano na wanaume hao watatu kisha wakaanza kumbaka kwa zamu.Wanaume wote hao ni wanafanya hospitalini hapo.