Marekani yasema imefanikiwa dhidi ya IS

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mmoja ya wapiganaji wa Dola ya Kiislamu ( Islamic State)

Mkuu wa majeshi wa Marekani amesema kampeni ya miezi mitatu dhidi ya dola ya kiislamu Islamic State imekuwa na mafanikio, lakini akaonya Marekani na washirika wake walikabiliana na ugumu pamoja vikwazo kwa muda mrefu.

Naye Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Chuck Hagel akizungumza kwenye bunge la congress amesema dola ya kiislamu imedhibitiwa na hivyo haiwezi kusonga mbele na maeneo mengine imesambaratishwa japo wanaonekana kuendeleza ushawishi kwenye ukanda wa Iraq na Syria.

Mkuu wa kikosi cha majeshi ya Marekani Generali Jack Dempsey anakadiria idadi ya wanamgambo wa dola ya kiislam kufikia 31,000.

Marekani imekuwa ikifanya mashambulizi ya anga dhidi ya kundi hilo, ambapo pia limekuwa likitoa ushauri na mafunzo kwenye majeshi kwa majeshi ya Marekani.