Mkutano wa G20 kuanza Jumamosi Australia

Haki miliki ya picha
Image caption Mji wa Brisbane, Quensland umeandaa mkutano wa siku mbili

Viongozi wa dunia wanawasili nchini Australia kwa ajili ya mkutano wa G20 utakaoanza siku ya jumamosi wiki hii mjini Brisbane.

Mkutano huo wa siku mbili ambao utawahudhuriwa pia na Viongozi wa Marekani, China na Urusi utaangazia maswala ya utangenezaji wa ajira, namna ya kubaini udanganyifu kwenye maswala ya ushuru na kuimarisha uchumi wa dunia.

Uhusiano kati ya Urusi na Ukraine pia utaangaziwa, huku wanaharakati wakitaka suala la mabadiliko ya hali ya hewa kuwa miongoni mwa ajenda.

Wafanyakazi wa Serikali mjini Brisbane wako mapumziko leo kutokana na changamoto za usafiri mjini humo.