Marekani kuunga mkono demokrasia Myanmar

Image caption Rais Obama na kiongozi wa Upinzani Aug San Su Kyi nchini Myanmar

Kiongozi wa upinzani wa Myanmar's , Aug San Suu Kyi, ameelezea imani yake kwamba Marekani itaendelea kuinga mkono juhudi za kuimarisha democrasia katika nchi hiyo iliyokuwa ikiendeshwa kwa utawala wa kijeshi kwa zaidi ya nusu karne.

Akiongea kwenye mkutano wa pamoja na rais Barack Obama huko kwao Yangon, Aug San Suu Kyi amesema japo mabadiliko yanafanyika katika hali ngumu ameiomba Marekani isilegeze msimamo wake.

Akikubaliana na kauli hiyo rais Obama amesema ni sharti juhudi zaidi ziongezwe ili kupata ufanisi zaidi wa kidemocrasia.

Marekani tayari iliuondoshea vikwazo vya kiuchumi utawala wa nchi hiyo licha ya hatua halifu za mabadiliko.

Aung San Suu Kyi amesema ni jambo lisilokubalika kuwa angali anazuiliwa kuwania uongozi wa nchi hiyo kwa sababu watoto wake walizaliwa ng'ambo.